Habari za Punde

*THE GOLDEN VOICE KUKAMILISHA MIKOGO

Nasri akiwa na Mpenzi wake wakipozi kwa picha



Na Sufianimafoto, Jijini Dar es Saam.

KUNDI jipya la miondoko ya Bongo Felva linalokwenda kwa jina la Sauti ya Dhahabu ‘The Golden Voice’ linatarajia kukamilisha video ya wimbo wao mpya uitwao Mikogo.
Mtunzi wa Wimbo huo, Nassor Ayub ‘Nasri’ alisema kuwa wimbo huo utakuwa hewani wiki ijayo baada ya kukamilika video hiyo katika studio ya Kazi One, ya jijini Dar es Salaam.
Aidha alisema kuwa katika wimbo huo pia amewashirikisha baadhi ya wanamuziki maarufu wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya, waliopo katika kundi hilo ambao wameweza kuonyesha uwezo wao wa hali ya juu.
Awali Nasri aliwahi kutamba na kibao chake cha Kizizi, kilichowateka kwa kiasi kikuba mashabiki wa miondoko hiyo na hata wazee kutokana na mashahiri aliyoyatumia katika wimbo huo.
Ikiwa ni kama miaka miwili kama si mitatu toka Nasri apotee katika anga za muziki wa Bongo Flava, mara tu baada ya kuibuka na kiabao hicho cha Kizizi sasa Nasri amepania kurudi kwa kasi ya ajabu ambapo ameanza na kibao hicho cha Mikogo, ikiwa ni maandalizi ya albam ya kundi hilo itakayokuwa na jumla ya nyimbo nane.
“Sijutii kukaa kimya kwa muda mrefu ama kupoteza mashabiki wangu, kwani mambo mazuru hayataki haraka na ndo maana nilikuwa najipanga kutoka kivingine zaidi na kazi zangu najipanga kuzifanya kimataifa zaidi sio ilimradi kufyatua kazi kwahi kuuza, kama wafanyavyo baadhi ya wasanii kuwa na albam tatu hadi nne lakini hata nyumba huna”. Alisema nasri.
Kutokana na kuwa kimya kwa kipindi kirefu, Nasri alisema kuwa baada ya kurekodi wimbo huo wameamua kukamilisha video ya wimbo huo ili kutambulisha upya ujio wa kundi lao kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Flava.
“Mbali na wimbo huo pizi zipo nyimbo nyingi tulizokwishaziandaa, ambazo tutazitoa mara tu baada ya kuachia kazi hii ya Mikogo ambayo naamini itafanya vyema katika jukwaa na muziki wa Bongo Flava” alisema Nasri.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.