Habari za Punde

*RAIS JAKAYA KIKWETE AKABIDHIWA JEZI YA RONALDO



















Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mstahiki Adam, Kimbisa akimkabidhi Rais Jakaya Kikwete, zawadi ya jezi namba tisa ya Timu ya Real Madrid ya Hispania inayovaliwa na nyota wa timu hiyo Ronaldo, wakati wa hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa kutambua mchango wa Rais Kikwete katika kukuza mchezo wa soka nchini. Picha na Freddy Maro-Ikulu

Msanii Paul Ndembo ambaye amejikita katika uchoraji wa sura za watu mbalimbali maarufu, hususan viongozi akimkabidhi, Rais Jakaya Kikwete, picha aliyoichora sura yake, wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.



Msanii Paul Ndembo (kushoto) akimuonesha Rais Kikwete moja ya picha alizochora za nyakati mbalimbali za Uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Picha hiyo imewekwa katika ukuta sehemu ya mapokezi Ikulu jijini Dar es Salaam. Msanii Paul Ndembo ni Mhitimu katika Kitivo cha Sanaa cha Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda Mwaka 1970 na ni mchoraji mahiri wa stempu za barua Tanzania.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.