Habari za Punde

*YANGA YAISHUSHA DARAJA MORO UNITED

*NGASSA, MGOSI NGOMA DROO-NANI KUTWAA KIATU CHA DHAHABU?












Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kulia) akimiliki mpira mbele ya Beki wa Moro UTD, Stephano Mwasika, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa uhuru Dar es salaam. Yanga ilishinda 3-0, huku Ngassa akitupia mawili na kufikia idadi ya magoli ya mshambuliaji wa Simba Mussa Hassan 'Mgosi'. Hivyo mpaka sasa wanaume hao wanafungana kwa idadi ya magoli kila mmoja akiwa na magoli 14. kitendawili kimebaki kwa mashabiki wanaojiuliza ni nani kati yao atatwaa kiatu cha dhahabu msimu huu wa ligi utakapomalizika ambapo kila timu ikiwa imebakiza michezo miwili. Yanga ikiwa imebakiza mchezo dhidi ya watani wao Simba, pamoja na Prisons, huku Simba nao wakiwa wamebakiza mtanange baina yao na watani wao Yanga, pamoja na Mtibwa.












Mrisho Ngassa, akishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Moro United, na kumuacha kipa wa Moro, Mohamed Bushiri, akigaa gaa, katika mchezo huo wa ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwana wa Uhuru Dar es Salaam leo jioni. Yanga ilishinda 3-0, huku goli ta tatu likifungwa na Boniface Ambani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.