Mpigapicha wa gazeti la Uhuru, Bashir Nkoromo, akimkabidhi simu ya mkononi, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Tumaini, Julieth Mushi, baada ya kufanya mawasiliano ya muda na kukutana nje ya Hoteli ya
ya Millenium Tower Makumbusho Dar es Salaam jana mchana. Mwanafunzi huyo aliangusha simu yake aina ya Nokia, wakati walipokuwa wakisafiri na kuketi siti moja na mpigapicha huyo, ambapo imeelezwa kuwa Jully alipanda gari hilo eneo la Bamaga wakati likielekea Kariakoo, huku akiwa ameongozana na mwenzake na wakatelemka Kituo cha Kinondoni B, kuelekea Chuoni.
Baada ya wanafunzi hao kutelemka, Bashiri aliona simu hiyo ikiwa katika siti na kuiokota na kisha kuihifadhi hadi alipopigiwa na mwanafunzi huyo kupitia simu ya rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Doris Valentine, na kuhakikishiwa na mwandishi huyo kuwa asiwe na wasiwasi ataipata simu yake na ndipo yakaanza mawasiliano hadi walipoonana na kumkabidhi simu hiyo ambapo Jully alionekana kufurahi zaidi na kutoamini imani ya mwandishi huyo huku akibaki kumwangali mara mbili mbili. Jamani Tuwe na imani kama hizi unapookota simu ya mwenzako jitahidi kumrejeshea kwani hujui madhara ya kumkosesha simu japo kwa dakia 1, ama contact anazokuwa amehifadhi na hujui ana mipango gani kwa siku hiyo ambayo anaweza kuipata kupitia simu yake, Simu ni kitu kidogo sana hata kama inagharama ya 100,000 na zaidi bado huwezi faidi kitu bali ni kujichumia dhambi tu.

Mimi binafsi hivi karibuni nimepoteza simu yangu wakati nikiwa kazini Uwanja wa Uhuru nikipiga picha za mchezo wa timu ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars na Ethiopia, na simu yangu wala haikuwa ya gharama sana bali yaliyokuwamo katika simu hiyo yalikuwa ni ya gharama kuzidi hata simu hiyo ambayo siku ya pili tu nilifanikiwa kununua nyingine lakini bado nikwa na machungu ya contact zangu na document nilizopoteza katika simu hiyo.
Naamini hata atakayekuwa ameokota simub hiyo ni miongoni mwa wenzangu niliokuwa nao eneo hilo ila imani iliwatoka na kuamua kuizima muda huo huo jambo ambalo kweli lilinisikitisha. Jamani kwenda kuhiji hatuwezi lakini hata imani basi........
"Asante sana Kaka kwa kweli wala siamini kama unaimani kama hii, mungu akusaidie uendelee na imani hiyo hiyo"
Bashir, akikumbatiana na Jully kwa furaha, baada ya kukabidhiana simu hiyo.
"Teh Teh Teh Teeeee! wala usijali dada hivyo ni vitu vya kupita tuu, na pia najua umuhimu wa simu"
Bashiri akiagana na Jully, baada ya furaha zilizojiri eneo hilo kwa muda mchache wakati wa makabidhiano hayo.
No comments:
Post a Comment