jana, Madega alizungumza na waandishi wa habari na kumponda Cannavaro na Mrisho Ngassa, huku akidai kuwa walipojiunga Yanga walikuwa wakipapatikia posho za Sh 10,000 na mishahara
Kwa upande wake Cannavaro, alisema kwamba ni kweli amepata ushawishi wa kwenda katika klabu ya Azam na kukiri kwamba suala zima la maslahi ndilo atakaloliangalia katika jambo
“Napenda niseme kwamba nimefedheheshwa na kauli za Madega, ingawa nitaendelea kumpa heshima yake
Alipoulizwa zaidi kuhusu habari za kwenda Azam, Cannavaro alisema si jambo la kuficha, limezungumzwa
“Mimi ni mchezaji, lazima niangalie mambo yangu ya kesho, soka ina muda wake, tena mfupi mno na ni vyema suala la maslahi nikalipa nafasi yake
Alipoulizwa ni vipi anakuwa tayari kuihama Yanga, Cannavaro alisisitiza kwamba suala zima la kuihama au kutoihama Yanga linahusisha zaidi maslahi na si vinginevyo.
“Naipenda mno Yanga na naomba mashabiki waelewe hilo, nimeitumikia klabu kwa moyo mmoja kwa wakati wote, hilo kila mtu analifahamu, lakini naomba ieleweke kwamba mimi ni binadamu kama wengine, suala la maslahi nalipa nafasi yake, nani asiyejua hilo,’’ alisema.
Alisema kwamba hataki kuingia katika malumbano yasiyo na maana na Madega, lakini mashabiki wa Yanga wanatambua mchango wake na katika suala hili la maslahi pia wataendelea kuelewa nini anachokisimamia.
“Sijawahi kuwa na matatizo na mashabiki wa Yanga, wananielewa linapokuja suala zima la kuitumikia Yanga kwa moyo mmoja, lakini haya yanayojitokeza sasa wanayatambua, wanajua mimi ni binadamu kama wao na nina wajibu wa kuangalia maslahi yangu,’’ alisema beki huyo wa Stars.
Cannavaro alisema ataendelea kuipenda Yanga na anaamini anaungwa mkono na wana Yanga wengi na akawaomba waelewe kwamba pamoja na yote hayo suala la yeye kuendelea au kutoendelea kuichezea Yanga msingi wake unabaki kwenye maslahi.
“Maslahi yangu ni kitu cha kwanza, nashangaa tunapoanza kuzua zogo na kutumia lugha zisizofaa wakati kilichotakiwa kufanyika ni mazungumzo na mimi katika
Alisema kwamba haitokuwa sahihi kwake kujibizana na Madega, kwani mwisho wa yote ataonekana mtovu wa nidhamu, jambo ambalo si zuri na anachodhani njia nzuri ya kumaliza tatizo ni kufanyika mazungumzo ya faragha na si
Naye Mrisho Ngassa, alipoulizwa juu ya kauli iliyotolewa na Mwenyekiti huyo, wa Yanga, alisema kuwa hana la kusema wala kujibu zaidi ya kusema tu anamshangaa na kauli zake, " Unajua kwa upande wangu mie wala siamini kama haya niliyoyasikia yanaweza kutamkwa na Mwenyekiti kama yeye tena mwenye elimu yake lakini zaidi ya yote mimi namshukuru mungu tu kwani ndiye muweza wa kila jambo na ndiye hasa anayeniongoza kwa kila kitu hadi kufikia hapa nilipo na wala si mtu yeyote mimi naamini hivyo". alisema Nagassa.
No comments:
Post a Comment