Habari za Punde

*FRANCIS MIYEYUSHO AMCHAKAZA MKENYA KWA KO

Bondia wa Tanzania, Francis Miyeyusho (kushoto) akipambana na Anthony Kariuki wa Kenya wakati wa pambano lao la kimataifa la kirafiki la raundi 8, lililofanyika kwenye Ukumbi wa DDC Kariakoo mwishoni mwa wiki. Francis alishinda pambano hilo kwa KO, katika raundi ya saba ya mchezo huo.

Francis akiendeleza libeneke, hata hivyo Mkenya huyo aliwaacha mashabiki hoi baada ya kushambuliwa mfululizo kwa masumbwi ya nguvu yaliyomchanganya katika raundi ya kwanza bila majibu kiasi cha kuwafanya mashabiki kuamini kuwa Mkenya huyo asingeweza kufika raundi ya pili ama ya tatu, lakini amini usiamini Kariuki alikuwa ni nunda aliyeweza kuvumilia makonde na suluba zote hadi raundi ya saba aliposalimu amri na kuanguka kama mzigo.

Kariuki akitokwa na udenda baada ya kipigo......

Kariuki akipewa huduma ya kwanza na Kocha wake baada ya kudiwa katika raundi ya kwanza kwa makonde ya mfululizo bila majibu.

Konde likitua usoni kwa Kariuki....

Mashabiki wa Miyeyusho, wakishangilia kwa nderemo na vifijo wakati wa pambano hilo.

Bondia wa Kike, Pendo, akifuatilia kwa makini pambano hilo lililokuwa likiendelea ulingoni.

Waamuzi au Makamisaa wa mchezo wakiwa bize kuhesabu pointi.....

MAPAMBANO YA UTANGULIZI NAYO YALIKUWA NI MOTO.....
Bakari Mohamedi (kushoto) akipambana na Safari Mbegu pambano la raundi 6. Safari alishinda kwa pointi

Bondia Ibrahim Hassan (kushoto) akichapana na Ramadhan Kumbela pambano la raundi 6, katika pambano hilo, Kumbela alishinda kwa pointi.

Issa Chalamanda, akiwa chini bada ya kusukumiwa konde zito na Yohana Robert. Yohana alishinda.











No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.