Habari za Punde

JWTZ WAKAMILISHA UKARABATI WA RELI KILOSA

Mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo (mbele) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu Eng. Omar Chambo eneo la Kidibo Mpwa leo wakikagua eneo lililokamilika kukarabatiwa na jeshi hilo shupavu ambalo leo limekabidhi kwa Wizara ya Miundombinu sehemu ya reli ya kati iliyoharibiwa na mvua mwishoni mwa mwaka jana (dec 2009) kati ya maeneo ya Gulwe hadi Kilosa mkoani Morogoro. Ukarabati huo wa 68 km umegharimu shilingi 15.6 bilioni (tz), Jeshi la wananchi limekamilisha agizo la RaisJakaya Kikwete kulitaka kukamilisha ukarabati huo kwa haraka ili wananchi kuondokana na kero ya usafiri pamoja na kuiletea taifa mapato ya uchumi. Kwa wakati huu itaanza kutumika kwa treni za mizigo hadi itakapotangazwa rsami kuanza safari za abiria. leo mchana. Picha na MWANAKOMBO JUMAA-MAELEZO

mafundi wakeendelea na ukarabati wa reli hiyo eneo la Kidete leo.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.