Habari za Punde

*MAMA SALMA KIKWETE ATUA CHINA KUHUDHULIA MKUTANO WA WANAWAKE ULIMWENGUNI

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Sarah Kitokezi, (miaka 3), kama ishara ya kukaribishwa rasmi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa wa kimataifa wa Beijing nchini China, ambapo amefika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa siku tatu utakaozungumzia masuala ya wanawake ulimwenguni.Wazazi wake binti Sarah ni maafisa waandamizi katka ubalozi wa Tanzania nchini China. Picha Zote na John Lukuwi-MAELEZO

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoka nje ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Beijing, mji mkuu wa China, akifuatana na Balozi wa Tanzania nchini China, Ramadhan Omar Mapuri (kulia), aliyefika kumpokea na kushoto ni Bibi Esther Mkwizu, Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation, ambaye yuko kwenye msafara wa Mama Salma. Mama Salma Kikwete yupo nchini China kuhudhuria mkutano wa 'Global Summit on Women' unaofanyika nchini humo kuanzia kesho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.