Habari za Punde

*MKUU WA WILAYA ARUSHA KUSHUHUDIA KINYANG'ANYIRO CHA MISS ARUSHA CITY CENTER



Na Eliya Mbonea, Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Eng. Raymond Mushi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
kinyang’anyiro cha Vodacom Miss Arusha City Center inayofanyika kesho katika ukumbi wa
hoteli ya Naura Springs.
Akifafanua katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi huo, Mkurugenzi
wa Sophy Entertainment, Sophia Urio ambao ni waandaaji wa kinyang’anyiro hicho alisema kuwa
kwa sasa wamejipanga vyema.
“Tunashukuru sana waandishi wa habari ambao wamekuwa bega kwa bega na sisi katika
kufanikisha hilo ambalo linatarajiwa kuanza kesho saa 1 usiku na kumalizika saa 6 usiku.
Kampuni yetu ndiyo ya kwanza kwa mkoa wa Arusha kufungua mashindano ya Vocodacom Miss Arusha
City Center na kufuatiwa na vitongoji vingine.
“Tunamshukuru Mungu tumepata washiriki wenye mvuto mbele ya jamii na tunaamini shindano letu
litakuwa na ushindani na msisimo”. Alisema Sophia”.
Kwa sasa tunao warembo 11 hao wapo kambini wakijinoa tayari kujiandaa kwa ajili ya
mashindano hayo.
Mataji yatakavyoshindaniwa ni Vodacom Miss Arusha City Center na Balozi wa Naura Springs
Hotel.
Wasanii watakaotumbuiza katika onyesho hilo ni Kikundi cha ngoma za asili kiitwacho Perfect
Youth Group, Bendi iitwayo Aqua Sound na wasanii wengine ni Hussein Machozi huyu ni msanii
wa hapa Tanzania.
Tunawashukuru sana wadhamini wetu ambao ni Vodacom, Naura Spring Hotel, Little Roses, Aqua Sound, Shuphaa Quality Boutique, Janneth Beauty Parlour.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.