
Wafanyakazi wa duka la Nafaka lililopo pembezoni mwa barabara ya Old Bagamoyo, eneo la Darajani karibu kabisa na TMJ, akiwa nje ya duka hilo huku wakijisomea magazeti kutokana na duka lao kuzingilwa na maji ya mvua kiasi cha kuwafanya wateja kukosa mahala pa kupita ili kujipatia huduma kwenye duka hilo.

Mkazi wa jijini Akipita kwa taabu katika barabara hiyo eneo la Darajani huku akiwa hana uhakika na safari yake kutokana na kutoona mwisho wa barabara hiyo jinsi maji hayo yalivyojaa.

Hii pia ni moja ya ofisi iliyopo pembezoni mwa barabara hiyo ikiwa imezingilwa na maji.

Hii ndiyo hali halisi ya maji katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment