Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 15, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Imani Madega, ikiwa ni zawadi ya mshindi wa pili katika msimu uliopita. Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephraem Mafuru
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akimkabidhi zawadi mchezaji wa Yanga Abdi Kasim kwa niaba ya Mrisho Ngassa, kwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu uliopita, wakati wa haflka ya kukabidhi zawadi za washindi kwa timu na wachezaji wa Ligi Kuu waliofanya vizuri. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraem Mafuru.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. milioni 10, Mwenyekiti wa Klabu ya Azam Fc, Said Mohamed, kufuatia timu hiyo kuwa mshindi wa tatu katika msimu uliopita
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera, akimkabidhi Tuzo ya kuwa Mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Oden Mbaga, wakati wa hafla ya kukabidhi zawdi kwa vilabu na wachezaji waliofanya vizuri katika msimu uliopita.
Katibu Mkuu wa Klabu ya Simba, Mhina Kaduguda, akiwa amepozi katika meza ya pekeyake baada ya kuingia katika hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Ligi Kuu iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. Haikuweza kufahamika sababu za Katibu huyo kufika na kuamua kuketi pekee hali ya kuwa meza nyingine walikuwapo viongozi wenzake wa Simba pamoja na wa vilabu vingine
No comments:
Post a Comment