Habari za Punde

*WANANCHI WA MBEZI JUU WALINDA ENEO LISIUZWE NA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA HUO

Vijana, wakazi wa Mbezi juu Kata ya Mtoni jijini Dar es Salaam, wakiwa na mabango, wakitoka katika eneo linalodaiwa kutaka kuuzwa na mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo. Vijana hao wamejitolea kulinda eneo hilo ili lisiuzwe kwa aliyedaiwa kuandaliwa kununua na kumilikishwa eneo hilo ambalo ni maalum kwa ajili ya kujenga Hospitali, Shule na Kituo cha Polisi ikiwa ni sehemu ya maendeleo ya wananchi wa mtaa huo
Baadhi ya viajana waliojitolea kulinda eneo hilo kwa niaba ya wanachi wa maeneo hayo, wakihojiwa na mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV, Henry Mabumo, wakati alipofika katika eneo hilo na kuwakuta wakiwa na silaha na mawe, wakidai kuwa wameanza ulinzi huo baada ya kupata taarifa kuwa mwenyekiti huyo amemuandaa mtu asiyejulikana ili kumuuzia eneo hilo lililobaki baada ya lile la kwanza kuuzwa na mwenyekiti huyo na kumpandikiza kuwa ndiye mmiliki wa eneo hilo ili aweze kujitangaza na waweze kung'oa alama zilizokwisha wekwa na wananchi ambao tayari walikwisha sajili eneo hilo Ardhi huku taratibu za kupata Kibari bado zikiendelea.

Vijana wakiandamana na mabango katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.