Habari za Punde

*WANENGUAJI WA SIKU HIZI NI WACHEZA SUMO? KUACHA MATUMBO WAZI SIYO ISSUE

"Duh! kunengua koooote huku hata kuja kunitunza no, Au hawanioni nini nipandishe tena Tshirt iwe kitop nini?"Pamoja na agizo la Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kuwa ikikemea mara kwa mara kuhusu wanamuziki au wanenguaji wanaopanda jukwaani wakiwa nusu uchi, lakini bado baadhi ya wanamuziki wamekuwa wafanya makusudi tena ama kwa kuchana nguo zao ama kuzikunja ili waonyeshe miili yao, lakini hii si mbaya sana kwani kila kazi inamzuka wake inawezekana bila kufanya hivyo hawawezi kupata mzuka wa kushambulia jukwaa. Lakini basi baadhi ya wanenguaji tuangalie miili yetu kabla ya kukunja nguo zetu ili kuonyeshamambo fulani kama wanavyoonekana wanenguaji hawa wawili wa bendi hii ya Stono Mayasika. Huyu ni mnenguaji wa bendi mpya ya Stono Mayasika, aliyejulikana kwa jina la Queen Leila, hebu mcheki tumbo lake, eti akishambulia jukwaa wakati wa onyesho la bendi yao lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dar City View uliopo Mbezi Juu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Wanenguaji wa bendi ya Stono Mayasika, wakishambulia jukwaa na staili yao ya 'Mswaki Mswaki', wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dar City View Mbezi Juu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Huyu naye mcheki hili tumbo nazani hajijui jinsi alivyo, sizani kama angeliacha tumbo hili wazi namna hii.

Wanenguaji hao wakishambulia jukwaa na staili yao ya Mswaki Mswaki.
Wanamuziki wa kiume wa bendi ya Stono Mayasika, wakishambulia jukwaa na staili yao ya 'Mswaki Mswaki', wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Dar City View Mbezi Juu jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mbona wanamuziki wanaume hawavai wala kucheza nusu uchi kama dada zetu?





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.