Habari za Punde

*BILALI ARUDISHA FOMU ZA KUWANIA URAIS ZANZIBAR

Mgombe urais kwa tiketi ya CCM, katika visiwa vya Zanzibar, Dk. Mohamed Gharib Bilali,
akizungumza na wananchi katika Viwanja vya Mwembesonga Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini
Magharibi, baada ya kutoka kurudisha fomu katika Ofisi za CCM Makao Makuu zilizopo
Kisiwandui, mjini humo.

Mohamed Gharib Bilali, akisalimiana na wanachama wa CCM, waliofika kwenye Ofisi za Makao
Makuu ya Chama hicho zilizopo Kisiwandui, mjini Zanzibar kumsindikiza kurejesha fomu ya
kugombea nafasi ya urais jana.

Wananchi wakiimba kwa furaha wakati wakimpokea Bilali alipokuwa akiingia kwenye viwanja hivyo.

Maandamano ya pikipiki yalizunguka mji mzima wakati wa hafla hiyo na shambla shambla za kumsindikiza Bilali kurudisha fomu.

Dk. Bilali, akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye viwanja hivyo. Kulia ni mkewe, Zakhia Bilali.

Mshereheshaji wa hafla hiyo, akizungumza kabla ya kumkaribisha Bilali, kuzungumza na wananchi.

Wanachama wa CCM na Mashabiki wa Mgombea nafasi ya Urais kupitia tiketi ya CCM, wakishangilia na kucheza ngoma wakati wa mapokezi ya mgombe huyo Mohamed Gharib Bilali, alipokuwa anarejea kwenye Viwanja vya Mwembesonga baada ya kurudisha fomu za wania nafasi hiyo. Hafla hiyo ya mapokezi ilifanyika jana, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Wanachi wao ilikuwa ni furaha tu, wakicheza sebene la matarumbea na Rusharoho mpaka mwisho.

Dk. Mohamed Gharib Bilali, akiwa na wakeze, Zakhia Bilali (katikati) na Asha Bilali, wakati wakiomba dua kwa pamoja na wanachi baada ya kumaliza mazungumzo na wananchi.

Kila mwananchi aliyekuwapo eneo hilo aliinua mikono juu kumuombea Dk Bilali ili kufanikiwa kuwa Rais wa Visiwa hivyo vya Zanzibar, baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi na kutoa shukrani zake kwa kumchangia fedha za kuchukua fomu na kumkubari ama kumpendekeza kuwa rais wao wa awamu ijayo.

Raia pia hawakuwa nyuma katika kupata kumbukumbu za mgombea huyo, nahii inaonyesha ni jinsi gani mgombea huyo amekubalika na kila mmoja wa visiwa hivyo, ili baadaye kuwa na picha ya mheshimiwa si kitu kidogo.

Ustaadhi, akiomba dua baada ya Dk. Mohamed Gharib Bilali, kuzungumza na wananchi, ambapo
wananchi wote waliokuwapo eneo hilo, waliungana kuomba dua maalum kwa ajili ya mgombea huyo.

Hata watoto pia walikuwapo nao wakiomba dua ili kumpata Dk. Bilali kuwa rais wa visiwa hivyo.

Dk. Bilali, akiondoka kwenye Viwanja hivyo huku akilakiwa na kila mtu aliyekuwapo katika viwanja hivyo, kila mmoja akitamani japo kumgusa.

Wananchi wakijipanga na kuomba dua na kuacha njia ya kupita mgombea huyo wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo.

Dk. Bilali, akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake maeneo ya Mazizini, baada ya kutoka kurejesha fomu. Kushoto ni baadhi ya wazee waliomshinikiza na kumsapoti katika kuchukua fomu hiyo ya kugembea urais.

Dk. Biali akiwa katika picha ya pamoja na wazee wake wanaomsimamia kwa kila jambo ili kufanikisha suala hiyo.


















No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.