Habari za Punde

*JAMBAZI AUAWA ARUSHA AKIFANYA JARIBIO LA UHALIFU



Na Sufianimafoto Reporter, Jijini Arusha.
MTU mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, anayesadikiwa kuwa Jambazi wa kutumia
siraha, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi ya ubavuni na askari Polisi, wakati jambazi
huyo akiwa na wenzake walipojaribu kufanya tukio la kuvamia Kituo cha Mafuta kilichopo eneo
la Kimandolu mjini Arusha majira ya sa tano asubuhi leo. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoani wa Arusha,
alisema kuwa tukio hilo limetokea katika Kituo cha mafuta, wakati gari lililokuwa limebeba
majambazi hao lilipofika katika kituo cha mafuta cha TOTAL kwa lengo la kutaka kuvamia na
kufanya uhalifu na kuanza kufyatua hovyo risasi hewani baada ya kuwaona askari wa Pikipiki
wakikatiza katika eneo hilo.
Aidha aliendelea kusema kuwa baada ya kupata taarifa kwa raia wema Askari Polisi waliamua
kwenda kuweka doria katika eneo hilo na ghafla iliingia gari hilo la majambazi wapatao wanne
lililokuwa na namba za bandia.
Baada ya kushuka katika gari hilo, majambazi hao walianza kuelekea kuwaharasi wafanyakazi wa
kituo hicho na hatimaye askari walipofika kwa haraka eneo hilo ghafla mmoja kati ya
majambazi hao alianza kufyatua risasi hewani huku akiwaamuru wafanyakazi hao kulala chini na
ndipo askari walipofanikiwa kumjeruhi mmoja wao kwa kumpiga risasi ya ubavuni.

Jambazi huyo alianguka chini huku akiwa hajiwezi na baada ya kusachiwa alikutwa na Bastola
aina ya BROWNING CZ 83 yenye namba A27411 iliyotengenezwa CZECK, hatimaye jambazi huyo alifariki dunia baada ya kufikisha katika Hospitali ya Mkoa Mount Meru.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.