Habari za Punde

*MR 2 AJIDHAMINI POLISI BAADA YA KUKAMATWA LEO

By www.janejohn5.blogspot.com
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Mbilinyi Mr 2, leo amekamatwa na kuhojiwa na Polisi kwa saa kadhaa, wakati akifanya mkutano na wandishi wa habari katika Ofisi za Baraza la Michezo Tanzania, BASATA, ijulikanayo kama 'Press Talk'.
Imeelezwa kuwa msanii huyo alikamatwa na kupelekwa Kituo cha Polisi ambako alihojiwa kwa saa kadhaa na askari wa upelelezi akituhumiwa kumtishia maisha Ruge Mutahaba, katika wimbo mpya wa msanii huyo ujulikanao kama 'Aunt Virus' uliokamilika siku za hivi karibuni ambao umekuwa ukisambazwa mtaani katika Cds bila kupelekwa katika vituo vya Redio.
Akizungumza kwa njia ya simu Mr 2, amekiri kuwa alikamatwa na polisi na kuambiwa na polisi
hao sababu za kukamatwa kwake kuwa Kiongozi mmoja wa Redio Clouds, waliomtaja kwa jina kuwa ni Ruge, amemshitaki Polisi kuwa anamtishia maisha baada ya kuusikia wimbo wake mpya wa Aunt Virus.
Aidha Mr 2 alisema kuwa baada ya kukamatwa alipelekwa katika kituo cha polisi ambacho
hakukitaja na baada ya kuhojiwa aliweza kujidhamini na kuruhusiwa kuondoka hadi siku ya
Jumatano kwa ajili ya kumalizia mahojiano hayo.
Msaada kwenye tuta by www.janejohn5.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.