Habari za Punde

*KCB YATOA PUNGUZO LABEI YA HISA KWA WANAHISA WAKE



Na Sufianimafoto Reporter, jijini Dar es Salaam

BENKI ya KCB Tanzania imezindua promosheni ya kuuza baadhi ya
hisa zake chini ya bei ya awali lengo likiwa ni kukuza kiwango
cha mtaji wa kampuni hiyo kubwa kanda ya Afrika Mashariki ikiwa
rasilimali za dola za Kimarekani 2.6.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uuzaji huo wa hisa mshauri wa
masuala ya kibiashara wa benki hiyo Amish Gupta alisema kwamba
mpango huo mahususi umekuja ili pia uwawezeshe wanahisa wa KCB kununua hisa nyingi za benki hiyo.

Akifafanua Gupta alisema kuwa kwa sasa wateja, wadau na wanahisa wa benki hiyo watanunua hisa moja ya KCB Tanzania kwa bei 310/- kutoka 385/- bei iliyokuwa ikitumika katika kipindi cha wastani wa miezi sita iliyopita punguzo likiwa ni sawa na asilimia 21.

“Mpango huu unaotarajiwa kuanza rasmi Julai moja utakamilika Julai 23 mwaka huu na kwamba wanahisa waliofanikiwa kununua hisa za benki yetu kupitia kwa mawakala wetu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa punguzo la bei watatajwa Agosti 5 mwaka
huu,” alisema Gupta.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa alisema hisa zitakazonunuliwa zitatumika katika nchi zote ambako benki hiyo inatoa huduma na zinauzwa kwa wananchi wote hata waso wateja wa benki hiyo.

Alisema pesa zitakazokusanywa zitatumika kupanua wigo wa utoaji huduma nchini na sio kwenye matawi ya nje ili kuongeza kiwango cha utoaji mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na uendelezaji wa makazi.

“Punguzo hili la bei litakaloanza Julai 1 mwaka Dar es Salaam huu litafanyika kwa wakati mmoja na Rwanda , Kenya na Uganda, hivyo natoa rai kwa watu wote kuchangamkia mpango huu utakaowawezesha kuonesha ushindani wa kibiashara litakapoanza Soko la pamoja la Afrika Mashariki,” alisema Dk Mndolwa.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Tanzania Joram Kiarie alisema wamepanga kuifanya benki hiyo kuwa suluhisho la masuala ya kifedha kote inakotoa huduma zake.

Alisema kwa sasa benki hiyo imetoa fursa kwa wateja kupata huduma za kibenki bila shida yoyote. Huduma hizo ni zile zinazolenga aina zote za wateja wakiwemo wafanyabiashara,
taasisi za serikali, mashirika mbalimbali, watu binafsi wakiwemo watoto.

Tofauti na hayo pia imeendeleza utamaduni wa kuwawekea akiba ya amana Watanzania kupitia mfumo wa benki ya Kiislam, benki kwa ajili ya wafanyabiashara, Ushirika pamoja na wateja wa kawaida. Pia kupitia huduma za Western Union , KCB pia inawawezesha wateja wake kutuma na kupokea fedha kwenye zaidi ya nchi 300 duniani.
Waandishi wa habari wakiwa bize kufuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo.
Mmoja kati ya wawekezaji wa benki hiyo, Amish Gupta, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi na kutambulisha huduma mpya yakutoa punguzo la bei ya Hisa kwa wanahisa wa benki hiyo, na mtandao wa kutoa huduma kwa wananchi wa Afrika Mashariki na Kati, ambapo mteja wa benki hiyo anaweza kutoa pesa za nchi aliyopo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Dr. Edmund Mndolwa, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wa uzinduzi na kutambulisha huduma mpya yakutoa punguzo la bei ya Hisa kwa wanahisa wa benki hiyo, na mtandao wa kutoa huduma kwa wananchi wa Afrika Mashariki na Kati, ambapo mteja wa benki hiyo anaweza kutoa pesa za nchi aliyopo.

Dr. Mndolwa akiteta jambo na mmoja kati ya watu waliohudhulia hafla hiyo, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Kivukoni, katika Hoteli ya Moven Pick jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.

Baada ya mkutano huo ilikuwa ni furaha na kubadilishana kadi kwa ajili ya mawasiliano ya kibiashara zaidi.

Hapa ni kubadilishana kadi tu kama huna haina kuandikiana kwenye karatasi.....

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia hafla hiyo wakijisevia maakuli.....

Kama kawaida kujisevia haikua issue........

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki hiyo wakiwa bize kusikiliza yanayosemwa mbele....










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.