Habari za Punde

*MAMA SALMA AZINDUA UPANUZI WA UKARABATI WA SEKONDARI YA TABORA WASICHANA

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiwahutubia mamia ya wanafunzi wa shule za Sekondari za Mko wa Tabora wavulana na wasichana na Mirambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari Tabora wasichana uliofanyika jana mkoani humo. Picha Zote na John Lukuwi-MAELEZO
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi (Rehabilitation and extension) wa shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora unaofanywa kwa hisani ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.7. Kushoto Mkuu wa Shule hiyo Ms Agness Mlelwa (kulia) ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa.
Mama Salma Kikwete akitembelea moja ya bweni lililokarabatiwa katika shule ya wasichana ya Tabora baada ya kuzindua mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule hiyo.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono kuwaaga wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora (wavulana na wasichana) na Milambo walihudhuria sherehe za upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari ya wasichana Tabora jana.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.