
Bendi ya TOT Plus, imeanza Bonanza laeke la kila jumapili katika uwanja wa Pub iliyopo njia ya Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaa, ambapo mtazamaji hushuhudia onyesho la bendi hiyo bure bila kulipa kiingilio bali anatakiwa kujihudunia kinywaji pekee. Huyu ni rapa na mwimbaji wa bendi hiyo, Jua Kali, akighani rap za bendi hiyo wakati wa onyesho lao la jana kwenye viwanja hivyo, ila mashabiki wa bendi hiyo wamekuwa wakijiuliza na kujishauri kunywa maji ya bendera ya bendi hiyo kutokana na kuwa ya msimu wa uchaguzi pekee. Bendi hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwa kutunga nyimbo nzuri lakini imekuwa ikizimika kiana na kuibukia wakati wa mambo ya CCM ama uchaguzi na kuwapa hedeki mashabiki wake wanaojiuliza
BENDI HIYO NI YA UCHAGUZI TUU?

Mwimbaji wa kike wa bendi hiyo, Polyn Zongo, (katikati) akiongoza safu ya waimbaji kushambulia jukwaa kwa kucheza miondoko ya bendi hiyo. Kushoto kwake ni Kiongozi wa bendi hiyo Badi Bakule 'Jogoo la Shamba'
No comments:
Post a Comment