Habari za Punde

*BALOZI WA SWEDEN NCHINI AMALIZA MUDA WAKE, AAGWA NA KUPONGZWA NA MCT

Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Justice Robert Kisanga, (kushoto) akimkabidhi Balozi wa Sweden nchini, Staffan Herrstrom, zawadi ya Fremu ya picha yenye sura ya Balozi huyo, wakati wa hafla ya kumuaga na kumpongeza baada ya kumaliza muda wake nchini, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Sea Clief jijini Dar es Salaam leo mchana, ambapo Balozi huyo amekula chakula cha mchana na Wahariri wa vyombo vya habari.


Balozi akifurahia zawadi ya kikapu cha asili baada ya kukabidhiwa.

Ilikuwa ni furaha na kutakiana afya njema baada ya makabidhiano ya zawadi.

Balozi akigonganisha grasi na baadhi ya Wakuu walioketi naye katika meza moja.

Balozi akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa na Baraza la Habari, baada ya shughuli hiyo kukamilika.

Balozi akizungumza jambo na Robert Kisanga (kushoto) Mark Bomani (wapili kulia) na Kajubi Mukajanga, wakati wa hafla hiyo.

Balozi akiagana na baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la habari wakati akitoka kwenye ukumbi huo.













No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.