Habari za Punde

*MAADHIMISHO YA MIKAKA 10 YA TWANGA YAFANA DAR

Rapa na mwimbaji wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta', Khalid Chokoraa, akiimba na kucheza na wanenguaji walioandaliwa rasmi kupamba ama kusherehesha maadhimisho hayo ya miaka 10 ya kazi za bendi hiyo, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam jana. Katika maadhimisho hayo kulikuwa na michezo mbalimblia ya soka baina ya timu na timu, ambapo mchezo wa mwisho wa kuwania seti ya Jezi ulikuwa ni kati ya timu ya waandishi wa habari za michezo Taswa Fc na Ile ya wanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta. Katika mchezo huo timu ya Twanga iliibuka kidedea kwa kuifunga Taswa Fc bao 1-0 bao lililofungwa na Idd Jenguo, katika kipindi cha kwanza cha mchezo bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

Pia kulikuwa na bendi zilizoalikwa kusindikiza maadhimisho hayo, kama Mafumo Bilali, OTTU Jaz Band, Profesa Jay, Dully Sykes, Nyadundo kutoka nchini Kenya na Kikundi cha ngoma cha Super Star By Coco cha jijini Tanga, pichani ni mwimbaji na rapa wa bendi ya Msondo Ngoma, Romario, akirap na kucheza miondoko ya bendi hiyo jukwaani.

Hawa ni baadhi tu mashabiki wa bendi hiyo waliojitokeza kushuhudia sherehe hizo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Hawa pia ni mashabiki wakifuatilia burudani jukwaani.

Wasanii wa kikundi cha Bay Coco, kutoka Tanga wakitoa burudani jukwaani.

By Coco jukwaani.....

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia miuno iliyokuwa ikimwagwa na By Coco jukwaani.

Mwimbaji wa Twanga, Rogatt Hegga Katapila akiwa na mashabiki wake akiangalia baadhi ya cd za kazi zao za siku za nyuma.

Hata wazungu pia walikuwapo, huyu ni mmoja kati yao akiwa na mtoto wake aliyemvisha Head Phone, ili kuzuia sauti kubwa ya spika za muziki kuathili masikio ya mtoto wake, huku akila koni na kufuatilia yanayojili jukwaani.

Mkuu wa Wiala ya Ilala, Leonidas Gamba, akizungumza, wakati wa hafla hiyo. Katikati ni Baraka Msilwa na Khadija Khalili.

Wanenguaji wa Twanga, wakishambulia jukwaa.

wakiendelea na mashambulizi.....

Mwimbaji, Kalala Junior, akipiga bass wakati wa sebene la kwanza la hafla hiyo....

Wanenguaji wa kiume wa Twanga, wakishambulia jukwaa...

Mnenguaji wa bendi hiyo, Lilian Internet, akiwa nje ya jukwaa akifuatilia kazi za jukwaani, Mnenguaji huyo imeonekana amekaa nje kutokana na kuwa mjamzito.

Ebwana eeh! kulikuwa na warembo wa kila aina na vivazi vya kila aina kama unavyowacheki warembo hawa ni baadhi tu wakifuatilia ya jukwaani kwa makini.

Katika kuhakikisha maadhimisho hayo yanakwenda vyema walialikwa pia wanamuziki na wasanii wa zamani waliowahi kupiti katika bendi hiyo wakatu huoooooo, ilipokuwa ikivuma na kibao cha Kisa cha Mpema, jukwani ni mwanamuziki Banza Stone, akiimba kibao cha Kisa cha Mpemba na (katikati) ni aliyekuwa mnenguaji wa bendi hiyo kwa kipindi hicho, Jobiso, ambaye kwa sasa anajishughulisha na Promosheni tu, (kulia) ni Luiza Mbutu.

Ikumbukwe bendi hiyo ilikuwa ikivuma hasa na mtindo wake wa Kutwanga na Kupepeta, na hawa ndiyo hasa walikuwa wakiufanyika kazi kwa kunogesha mashabiki wa bendi hiyo, hapa wakionyesha namna ulivyokuwa ukichezwa mtindo huo.

Kati ya wanenguaji hawa ni mmoja tu ambaye angalau alionja ladha ya mtindo huo wa kutwanga na kupepeta, Aisha Madinda wa kipindi hicho, ambaye kwa sasa anatumia jina la Aisha Mohamed, baada ya kuachana na aliyekuwa Boy Friend wake Fikiri Madinda, hapa wakicheza miondoko hiyo.

Banza Stone na Jobiso wakishuka jukwaani baada ya kumaliza kuimba vibao vya zamani.

Huyu si Beyonce, ila ni mnenguaji wa bendi hiyo, Queen Suzzy, ambaye pia alikuwa likizo kutokana na kuumwa, hapa akipozi kwa picha na mtoto wake pamoja na rapa wa Fm Academia, G 7 katika viwanja hivyo vya Leaders Club.

Professa Jay, (watatu kushoto) na Man X (wapili kushoto) wakipozi kwa picha na baadhi ya washkaji kabla ya Profesa kupanda jukwaani kuwapagawisha mashabiki wake lukuki waliopagawa vilivyo na kumtaka aendelee kutumbuiza tuuuuuuuu..........

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Leonidas Gamba, akimkabidhi zawadi ya Jezi na Vuvuzela , Mwenyekiti wa timu ya Waandishi wa Habari za michezo Taswa Fc, Majuto Omar, baada ya mchezo kati yao na Twanga. Kushoto ni Omary Baraka.

Mkuu wa Wialaya ya Ilala, Leonidas Gamba, akimkabidhi zawadi ya jezi, golikipa wa zamani wa timu ya Simba, Mohamed Mwameja.

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya, Nyadundo, akiimba jukwaani kwa staili ya kipekee na kutumia kinanda cha kupuliza kwa mdomo kiasi cha kuwapagawisha watu waliofurika kumtunza msanii huyo.

Mashabiki wa muziki wa Kijaruo wakicheza miondoko hiyo iliyokuwa ikiporomoshwa jukwaani na Nyadundo kutoka Kenya.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Professa Jay, akiwapagawisha mashabiki wake baada ya kupanda jukwaani.

Mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, wakipagawa na Profesa Jay, hadi mtoto huyu alikuwa ni mmoja wao kama unavyomuona eti pamoja na kubebwa naye pia ameinua mkono juu kuashiria anaburudika vilivyo na Profesa Jay.

Nao Mashabiki wa Dully Sykes hawakuweza vumilia nao walipanda jukwaani kumsapoti wakati akiimba kibao chake cha Shekide.....

Dully Sykes, akiwapagawisha mashabiki wake jukwaani.






























No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.