
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa mfumo mpya wa kudhibiti magari kwa kutumia mtandao maalum ‘Car Tracking System’ utakao kuwa na uwezo wa kuyaona magari yote yatakayokuwa yamejisajiri na mfumo huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wenye mabasi (TABOA) Mohamed Abdallah (wapili kulia) ni Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya uTRACK, Zully Mohamed na Ofisa Mipango Mkuu wa kampuni hiyo, Pirbaksh Ashraff.

Baadhi ya askari wasikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kamanda kuhusu mfumo huo.

Askari wa Usalama barabarani wakiwa kati hafla hiyo ya uzinduzi.

Pamoja na uzinduzi huo, lakini bado dosari za ofisi hizo zimeonekana wazi pale Bendera ya Jeshi hilo la Polisi, ikionekana kuwa nusu mlingoti tena muda wa mchana. Haikuweza kufahamika chanzo cha bendera hiyo kuwa katika muonekano huo. Jamani Wahusika hebu rekebisheni bendera hiyo isijeleta maana nyingine kwa wananchi.

Kama inavyoonekana ikiwa sambamba na Bendera ya Taifa nje ya Kituo hicho cha Polisi.
No comments:
Post a Comment