Meneja wa Kiwanda cha Murzah Oil Mills, Dinesh Khanna (kushoto) akimkabidhi Vifaa vya kuwasaidia kusikia wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Rosemary Lulabuka kwa ajili ya kukabidhi msaada huo kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Twiga ya Jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo fupi iliyofanyika shuleni hapo leo mchana, ambapo vimekabidhiwa vifaa vyenye thamani ya Sh. milioni 8.6 kwa wanafunzi hao.
Mwalimu Mkuu wa Kitengo cha Viziwi wa Shule ya Msingi Twiga ya Jijini Dar es Salaam, Rahel Kazeni (kulia) akimvisha kifaa cha kusaidia kusikia, mmoja wa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, Jordan Fwere, baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh. Million 8.6 leo. Kushoto ni mwakilishi wa Kiwanda hicho Sudhakar Sudhakar, (wapili kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Rosemary Lulabuka na watatu (kulia) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Joseph Mbezi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu, akipkea msaada ya vifaa hivyo kwa ajili ya kuwakabidhi wanafunzi wa Shule ya Msingi Mtoni. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Omary Kitwana.
No comments:
Post a Comment