Na Hastin Liumba,Urambo
WANACHAMA wa chama cha mapinduzi,(CCM),wilaya ya Urambo mkoa wa Tabora,wanaodaiwa kuwa ni wapambe wa Spika wa Bunge, Samweli Sitta, pamoja na walinzi wake wamedaiwa kuwashambulia wafuasi wa chama hicho na kusababisha mmoja kati yao kulazwa hospitali ya wilaya ya Urambo kwa maumivu makali.
Tukio ilo lilitokea julai 26, mwaka huu, majira ya saa nne na nusu, katika kijiji cha jionee, Kata ya Songambele Wilayani humo baada ya wafuasi wa mgombea ubunge wa jimbo hilo anayechuana na Samweli Sitta, Ali Maswanya, kuvamia mkutano uliokuwa umeitishwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Matheo Salu.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake walioshiriki tukio waliloliita la kuzima jaribio la kutoa rushwa katika kijiji hicho Haroub Sultan, alisema awali walipokea maelekezo ya wanachama wanaodaiwa ni wafuasi wanaomuunga mkono na kumfanyia kampeni Samweli Sitta,wakiongozwa na Mohamed Helis (Weli),ambaye pia ni mgombe udiwani kata ya Urambo mjini ambaye anadaiwa kuwa mpambe wa spika wapo kjiji hicho na wanapanga kukutana na wajumbe wa kamati ya siasa ya CCM kata ya Songambele.
Alisema kuwa baada ya kupokea taarifa hizo walipiga simu taasisi ya kuzzuia na kupambana na rushwa,(TAKUKURU), na kituo cha polisi,majira ya saa 03:30 usiku, kuelezea kuwa kuna wanachama wanaodaiwa kuwa wapambe wa spika Samweli Sitta wapo kijiji cha Jionee wanatoa rushwa y ash 10,000 kwa wanachama wenye sifa na kwamba awali walikuwa Songambele na walishakutana na baadhi ya wanachama na viongozi.
Hatua hiyo ya wapame hao wanaoaminika ni wa Sitta walikuwa wakikusanya wanachama wenye sifa za kupiga kura ya maoni kuelekea uchaguzi mkuu wa wabunge mwezi ujao.
Aidha baada ya kuttoa taarifa TAKUKURU na kituo cha polisi,walijibiwa kuwa watangulie na kamera wakawapige picha,na kwamba wao wanakuja kwani muda huo walikuwa wakitafuta gari ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Urambo.
Aidha anaeleza kuwa baada ya kuelezwa na TAKUKURU na kituo cha polisi waende kupiga picha walifanikiwa kwenda eneo la tukio wakiwa na gari lenye namba za usaji T 700 ASC na baada ya kufika katika tukio hilo,walikuta gari lenye namba za usajili za T459 BBV aina ya Toyota Landcrouser mali ya Hemed Halfani na pikipiki moja yenye usajili namba T 174 BCH huku baadhi ya watu zaidi ya saba wakianza kukimbia huku katikati yao kukiwa na mtu ambaye alikuwa akikingwa asifahamike kuelekea gizani .
Anafafanua kuwa baada ya kufika na kushuka ndai ya gari mbili walizokwenda nazo,akiwa na Kahise Sayumwe,Twaha Habib,Dotto Aman,Juma Mbalamwezi,Hummud Nasoro ambaye amelazwa baada ya kupigwa na mtwangio wa kinu na jembe kichwani,Bundala Huseein Kakema,Yahaya Kidagwe,Masoud Kalukanya na Mashaka,mwenyekiti wa kijiji cha Jionee Matheo Salu aliwanza kufoka akitamka nyinyi mmefuta nini hapa.
Sultani aliyekuwa akiongoza wenzake,alijibu mwenyekiti wewe muulize huyu,(mpambe wa Sotta),Mohhamed Weli yeye kafuata nini usiku ule pale kijijini wakati muda wa kampeni umepita na kwamba wao wametoa taarifa polisi kuwa wao wanatoa rushwa na kufanya kampeni usiku ule.
“Tumekuja hapa kuwataka muache mchezo mchafu wa kutoa rushwa na kufanya kampeni na kwamba hapa tupo tayari kwa lolote huku weli yeye akiwa naondoka na gari kuelekea mashariki.” Alisema Sultani.
Aidha alisema bada ya kuondoka na kuendesha gari kwa urefu wa kilomita zipatazo moja na nusu,waliona watu wasiopungua saba hivi wakiingia kwenye gari hilo lenye namba za usaajili za T 459 BBV likiondoka kwa kasi ya ajabu kuelekea mjini.
Sultani anasema kuwa bada ya dakika 10 hivi waliona gari mbili zikija kwa kasi walipo na baada ya kufikan walipo walizitambua kuwa ni gari za spika wa bunge Samweli Sitta ambapo baada ya kusimama walishuka walinzi wawili wa spika na kuliza “WAKO WAPI HAWA”.
“Mimi sikujificha nilijitokeza na kusema mimi hapa kabla ya milinzi mmoja kunipiga ngwara niadondoka chini na alinikany`aga na mguu wa kulia kifuani huku akisema “tutakumaliza” mnampigia kele mtu ambaye ni muhuni….hamtafanikiwa kamwe kwani hayupo kwenye “system” aliongeza Sultani ambaye anaeleza maneno hayo hata mahakamani atayarudia tu akifika huko.
Anasema wakati mabishano hayo yakifanyika mbele ya wananchi Mohammed Weli aliwaamuru baadhi ya wananchi waanze kuwashambua ndipo mapambano yalipozuka ambapo mwenzao mmoja wakati akikimbia kuingia kwenye gari alikamatwa na kushambualiwa nan jembe kichwani na kupigwa sehemu za mbavu kulia ambazo zimeivia damu na kupoteza fahamu baada ya kudondoka.
Alisema wakati hayo yakiendelea wananchi hao baada ya kupewa amri ya kutembeza bakora,pia walivunja gari kioo cha nyuma iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aitwaye Mashaka,huku yeye akiwa chini ya mlinzi wa spika Sitta akiwa kawekwa chini ya ulinzi mkali huku mlinzi huyo akiwa kachomoa bastola akitamka atampasua kichwa kwa risasi.
“Tulia wewe kijana mnampigia kampeni muhuni na sikilizeni huyo hata kama akishinda kura za maoni NEC haitaweza rudisha jina lake” alitamka maneno hayo milinzi wa spika mmoja.
Alisema muda huo alikuwa akilazimishwa kuingia kwenye gari nay eye akawa anagoma na kutaka hadi TAKUKURU na polisi watakapofika eneo la tukio kitu ambacho mlinzi mmoja wa spika Sitta alikiafiki.
Aliongeza kwamba baada ya polisi kufika eneo la tukio hilo wakiongozwa na OC-CID ambaye hamkumbuki jina ndipo taratibu za kipolisi zilifanyika huku mwenzao aliyezimia pale chini Hamudu Nassoro akiandikia barua ya kwenda kwa mganga mkuu wa hopitali ya wilaya kupata matibabu haraka.
Alisema katika barua hiyo ambayo ilikuwa na muhuri wa “Kituo cha polisi wilaya ya Urambo” kikiandikwa maneno haya ya “JESHI LA POLISI TANZANIA” HATI YA MATIBABU kilichoandikwa mwezi julai 27 mwaka huu kwenda kwa mganga mkuu urambo hospitali.
“Hati hiyo ya malipo ilisema hivi, MH: HUMUDI Nassoro ”Mtajwa hapo juu amepigwa tunaomba apatiwe matibabu kikiwa na sahihi na namba E 2131.
Gazeti hili lilikwenda upande wa pili kwa wahusiaka wanaotuhumiwa kutoa “mlungula” akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Jionee Matheo Salu na mbunge aliyemaliza muda wake Samweli Sitta lakini kwa juhudi kubwa iliyofanywa na mwandishi awa habari hii,hakupatikana kuzungumzia sakata hilo huku kukiwa na majibu ya kuwa wapo kwenye kampeni za uchaguzi huo.
Aidha msemaji wa TAKUKURU na polisi wilaya hawakupatikana,huku polisi wakitoa maelezo kuwa wao siyo wasemaji na kwamba kamanda wa polisi mkoa Liberatus Barllow ndiye msemaji wa sakata hilo.
Aidha kwa upande wa uongozi wa hospitali ya wilaya ya Urambo walishindwa kutoa maelezo yao kwa madai ya kwamba hadi wapewe kibali na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo,Justus Molay.
Katibu wa afya wa hospitali hiyo ambaye alidai kukaimu nafasi ya mganga mkuu wa wilaya hiyo B.Kalatwa alisema hana cha kujibu pamoja na kwamban kuna mwanaCCM aliyeletwa hapo kutibiwa.
Hamudu Nassoro akiwa hospitali ya Wialaya alipolazwa baada ya kuumia katika sakata hilo...
No comments:
Post a Comment