Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kuwashangaza abiria waliokuwa wamepanda boti za Kilimanjaro na wengine katika Boti ya Sea Express, ilikuwa ni kuona jinsi boti hizo zilivyokuwa zikikimbizana kutoka mjini Zanzibar kuja Dar ili kuwahi kupaki Bandalini. Boti hizo zote ziliondoka katika Bandari ya Zanzibar mida ya Saa 10 jioni kuja Dar huku ikianza kuondoka Boti ya Sea Express, ambayo ilisimama katikati ya bahari kwa ajili ya kutoa msaada kwa boti iliyokuwa ikielekea kuzama katika eneo fulani na kupitwa na Kilimanjaro. Boti hiyo haikuweza kuvumilia kwani iliikimbiza Kilimanjaro na kukaa nyuma kiasi kwamba ikashindwa kuvumilia mawimbi ya Kilimanjaro kutokana na utofauti wa boti hizo kwa ukumbwa na ndipo dereva wa Sea Expres alipoamua kuendesha boti hiyo kama dereva wa daladala ambao huitwa 'WaruWaru' kwani alipita pembezoni kabisa mwa Bahari na alipokaribia eneo la Msasani alipita nje ya Maboya yanayoonyesha mwisho wa njia ya boti na kuovateki na kisha kuingia kwa mbele na kufanikiwa kuwahi kupaki ikiwa ya kwanza.
Hivi ndivyo ilivyokuwa ikifanya boti hiyo hapa ilikuwa ikipita nje ya boya karibu kabisa na kingo ama mawe yaliyo pembezoni mwa bahari ya Hindi eneo la Msasani.
*LUMBESA SI BONGO PEKEE HATA ZENZI KAMA KAWA
Hata hivyo magari makubwa kama haya yanapokuwa na mizigo mizito husababisha foleni kubwa katika barabara za mijini hebu wahusika angalieni muda wa kuyaruhusu magari kama haya kupita katika barabara zinazotumiwa na watu wote.
Mkazi wa Mjini Zanzibar akisafirisha madumu matupu katika baiskeli yake kuelekea kuuza katika Soko la Darajani......
*HAYA SI MAGOFU BALI NI NYUMBA NA ZINAPANGISHWA NA SERIKALI YA ZANZIBAR Hizi ni nyumba za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, zilizopo Darajani mjini Zanzibar zinazopangishwa kwa wananchi kama ni hapa home waweza kusema NHC, lakini zikiwa hazina muelekeo wowpte wa kuzikarabati ama kuzibadilisha kutokana na kuchoka kwa majengo hayo. Hata kama ni mji wa Makumbusho lakini basi wakubwa wajaribu kuangalia ni jinsi gani wanaweza kuyaboresha na kuwa kivutio zaidi kwani ipo siku yataporomoka kabisa halafu makumbusho yatabai jina ni bora kuziba ufa kuliko kujenga ukuta.
*WAMASAI FEKI WAJAZANA ZANZIBAR WAZUGA NA KUUZA UREMBO MCHANA USIKU ULINZI KAMA KAWA Hawa ni baadhi tu kati ya Wamasai kibao waliojazana mjini Zanzibar katika maeneo mbalimbali, ambao usiku hugeuka kuwa walinzi wa mageti na nyumba za watu. Hebu mdau angalia watu hawa ni wamasai wa wapi hawa mcheki huyu wa katikati na ametoga sikio na panki la Kibrazamen kabisa Wakuu angalieni wamasai wa kuwaajali katika kazi ya ulinzi jamani ohooo!
No comments:
Post a Comment