Habari za Punde

*PPF YATOA MSAADA WA VYA KUHIFADHIA MAJI HOSPITALI YA WILAYA YA TEMEKE

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma PPF, Kanda ya Temeke, Lindi na Mtwara, Lulu Mengele (watatu kushoto) akimkabidhi risiti Mganga Mkuu wa Hospitali ya Temeke, Dk. Asha Mahita, ikiwa ni sehemu ya kukabidhi Sim Tank 2 zenye thamani ya Sh. milioni 2 kila moja likiwa na uajazo wa Lita 500 kwa ajili ya kusaidia tatizo la maji katika wodi ya wazazi na Chumba cha upasuaji wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika hospitalini hapo leo mchana, (kulia) ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa PPF, Sarah Kibonde Kushoto ni Muuguzi Kiongozi wa Kitengo cha Magonjwa ya nje (OPD), Nasekile Mwankenja.

Wakipiga picha ya kumbukumbu kwa pamoja baada ya makabidhiano hayo baina ya Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo na Meneja wa Kanda.

Ofisa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma PPF, Kanda ya Temeke, Linda Njoolay, akigawa sehemu ya msaada kwa Asha Arabi mkazi wa Mbagala Rangi 3 aliyelazwa kwenye Wodi ya watoto katika Hospitali ya Wialaya Temeke Jijini Dar es Salaam jana, wakati Meneja wa Lindi na Mtwara, Lulu Mengele na ujumbe wake walipofika hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya kuhifadhia maji (Sim Tank) mbili zenye thamani ya Sh. milioni 2 kila moja likiwa na uajazo wa Lita 500 kwa ajili ya kusaidia tatizo la maji katika wodi ya wazazi na Chumba cha upasuaji.

Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma PPF, Kanda ya Temeke, Lindi na Mtwara, Lulu Mengele, akifurahi na mtoto Janeth Gaudence, baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika wodi ya watoto hospitalini hapo leo mchana. Kushoto ni mama wa mtoto huyo, Editulda Gaudence.

Wauguzi na wafanyakazi wa PPF wakiwa bize kugawa sehemu ya misaada hiyo ndani ya wodi ya watoto.

Hawa ni baadhi ya wadau na waandishi wa habari waliohudhulia hafla hiyo kwenye Hospitali ya Wilaya ya Temeke leo.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.