Habari za Punde

*UCHAGUZI WA VIONGOZI CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI TASWA

Dina Ismail na Cecy Jeremiah ndani ya ukumbi.

Hapa wakicheka na kutaniana ‘Ebwana eeh! Hii nafasi niachine mie Kaka we si tayari umeshaitumikia kwa kipindi hiki tunachomaliza?’ Kitenge akisema.

Kitenge akiendelea kusalimiana na wagombea wenzake, hapa akisalimiana na Tom Chilala wanaogombea pamoja nafasi hiyo.

Wagombea hao wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya uchaguzi ambapo mmoja kati yao anatarajia kuchinjwa, Kati ya hawa ni mmoja tu atakayepita kwa kura za wanachama.

Wagombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Maulid Kitenge na Shafii Dauda, wakisalimiana ukumbini hapo kabla ya kuingia kwenye Chumba cha uchaguzi.

Mgombea nafasi ya Uenyekiti Mpoki Bukuku, anayechuana na Masoud Sanani na Juma Pinto, akiingia kwa mikogo katika viwanja hivyo vya ukumbi wa Manispaa Kinondoni huku akiwa na mabodgadi.

Ali Mkongwe na Mbozi Ernest wakipiga stori nje ya ukumbi huo.

Wanachama Ibrahim Maestro na Khadija Khalili, wakipiga stori nje ya ukumbi huo.

Baadhi ya wanachama wa Taswa na wagombea wakiwa nje ya Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, wakati wakibiri kuingia ukumbini kuanza uchaguzi huo.

Mgombea wa nafasi ya Mweka Hazina msaidizi katika Chama cha Waandishi wa habari za michezo TASWA, Dina Ismail, akipiga magoti mbele ya wapiga kura ili kuomba kupigiwa kura katika uchaguzi huo unaotarajia kuanza muda mchache kuanzia sasa.










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.