Habari za Punde

*CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TASWA CHAPATA VIONGOZI WAPYA

Mwenyekiti mpya wa Chama cha waandishi wa habari za michezi Tanzania, Juma Pinto,
akizungumza baada ya kutangazwa matokeo naye kuibuka kidedea kwa kuwamwaga wapinzani wake Masoud Sanani aliyepata kura 11 na Mpoki Bukuku, aliyepata kura 8 tu.
Wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti kutoka (kushoto) Shafii Dauda, Maulid Kitenge na Tom Chilala, wakishikana mikono ikiwa ni ishara la mshikamano na umoja wakati wakimpongeza
mwenzao Maulid Kitenge baada ya kutangazwa matokeo ambapo Kitenge aliibuka kidedea kwa kura 37 kati ya kura 79 zilizopigwa, akifuatiwa na Shafii aliyepata kura 31 huku nafasi ya mwisho
kati ya wagombea hao ikichukuliwa na Tom Chilala aliyejipatia jumla ya kura 11.

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, Mpoki Bukuku, akijinadi mbele ya wanachama kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo.

Duh! Sijui watanimwaga?
Nasongelya akiwa na mawazo lukuki wakati wa zoezi hilo likiendelea.
HII ILIKUWA NI KAMPENI YA UKAILA AMA?
Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Shafii Dauda (kushoto) akijadiliana jambo na Mahmud
Zubeir na Timzoo Kalugila wakati zoezi la kupiga kura likiendelea ukumbini humo.

Baadhi ya wananchama wakiwa kwenye foleni ya kwenda kupiga kura, huku mmoja wao akiwa
amevali Tshirt yenye ujumbe madhubuti kuhusiana na uchaguzi unaohamasisha kuchagua viongozi walio Bora

Mgombea aliyeibuka kidedea katika nafasi ya Uenyekiti, Juma Pinto, akijinadi kwa wanachama
kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo.

Baadhi ya Wajumbe na wanachama wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo, Taswa, wakiwa kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati wa mchakato mzima wa kuchagua viongozi wapya wa chama hicho, ambapo uchaguzi huo umeweza kufanyika na kumalizika kwa amani.

Mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Tom Chilala, akijinadi mbele ya wanachama ili kuomba kura kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo.

Viongozi waliomaliza muda wao ambao baadhi yao wamefanikiwa kurudi katika nafasi
walizogombea na wengine wakiwa wameanguka vibaya.

Mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, Masoud Sanani, akitafakari kura atakazopata kabla ya
kutangazwa matokeo ambayo yalimwangusha baada ya kuibuka na jumla ya kura 11 kati ya 79
zilizopigwa.

Mgombea nafasi ya Ujumbe Zena Chande akiwa na mawazo lukuki kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo.












No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.