Habari za Punde

*WAREMBO WA MISS TZ 2010 WAINGIA KAMBINI LEO, KUANZA MBIO ZA KUMRITHI MIRIAM GERALD

Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Miss Tanzania 2010-2011, wakiwa kwenye gari kelekea katika Hoteli ya Grrafe Ocean View Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam, kuanza Kambi kwa ajili ya maandalizi ya shindano la Taifa linalotarajia kufanyika hivi karibuni.
Warembo hao wakiingia kwenye gari lililoandaliwa kwa ajili yao kuelekea kambini.

Warembo hao wakitoka nje ya ofisi za Miss Tanzania walikokutana leo mchana kwa maandalizi ya kuelekea kambini.
Waremboa hao wakiwa ndani ya ofisi za Miss Tanzania, wakisubiri kukamilika kwa taratibu za kuanza safari.
Miss Tanzania 2010, Miriam Gerald, akipozi kwa picha na mchambuzi wa michezo Edo Kumwembe katika ofisi za Miss Tanzania wakati wakisubiri usafiri wa warembo.
Baadhi ya warembo wakijadiliana na kupiga stori ndani ya ofisi za Miss Tanzania leo.
Pozi la mwisho la warembo ndani ya ofisi za Miss Tanzania.


Na Sufianimafoto Reporter, jijini

Warembo waliofanikiwa kuingia Fainali ya Taifa ya Mashindano ya Urembo ya VODACOM MISS TANZANIA 2010, leo wameingia kambini kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumrithi mrembo anayemaliza muda wake, Miriam Gerald.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo mchana kabla ya warembo hao kuelekea Kambini, Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, alisema kuwa “Warembo hao Wakiwa kambini watakuwa na ratiba mbali mbali ikiwa ni pamoja na kufanya kazi za kijamii na kutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya kitalii”

Alizitaja sehemu hizo kuwa siku ya Tarehe 17 / 08 / 2010 warembo watapewa semina maalumu na viongozi wa kamati ya Miss Tanzania pamoja na kusaini mikataba kati yao na waandaaji.

Tarehe 19 / 08 / 2010 waandishi wa habari wote watapata nafasi ya kuongea na washiriki na kupata maoni yao na jinsi walivyojiandaa katika kunyakuwa taji la VODACOM MISS TANZANIA 2010

Mwishoni mwa wiki warembo wote wakiambatana na baadhi ya viongozi wa kamati watasafiri kwenda katika mikoa ya kanda ya kaskazini “KILIMANJARO: na “ARUSHA” kwa ajiri ya kutembelea vivutio vya utalii ili kuvitangaza na kuwahamasisha watanzania ili wajenge utamaduni wa kutembelea, kuvilinda na kuvithamini vivutio vyetu.

Huu ni mpango tunaoshirikiana na taasisi za serikali yaani ,BODI YA UTALII, TANAPA na NGORONGORO CONCERVATION AREA AUTHORITY.

Huu ni mwaka wa pili taasisi yetu “Miss Tanzania” kushirikiana na taasisi za serikali kuhamasisha watanzania kuthamini na kutembelea vivutio vilivyopo nchini kwetu.

Tunategemea kwenda mbele zaidi kwa kuvitembelea vivutio vya kusini mwa Tanzania, SELOUS, RUAHA NATIONAL PARK, MIKUMI na UDIZUNGWA, katika siku za usoni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.