Habari za Punde

*TUZO ZA TAIFA ZA UGUNDUZI ZATOLEWA LEO DAR

Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla akimtunuku cheti cha kuwa mshindi wa kwanza Prof. Mathew Luhanga wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam baada ya Taasisi ya Kompyuta ya Chuo hicho kushika nafasi ya kwanza ya ugunduzi na ubunifu na kuwa watafiti mwaka wa 2010, wakati wa sherehe ya kutoa tuzo hizo za Taifa zilizofanyika Jijini leo mchana.
Waziri wa Sayansi na Teknolojia Prof. Peter Msolla, akiangalia mbegu za mahindi na kupata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Kilimo wa kituo cha utafiti Ilonga kilichopo Kilosa mkoani Morogoro Dk. Chaboba Mkangwa. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia Dk. Hassan Mshindi.
Wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine -Morogoro (SUA) Prof. Rhodes Makundi (kulia) na Christophe Cox (kushoto) wakitoa maelezo ya panya buku wenye uwezo kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini na vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu (TB) leo jijini Dar es salaam wakati sherehe ya kutoa Tuzo za Taifa za Ugunduzi na Ubunifu pamoja na utoaji wa fedha za kusaidia shughuli za utafiti wa elimu, kilimo,ufugaji, ufundi na viwanda kwa taasisi na vikundi mbalimbali nchini .



No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.