Habari za Punde

DK. BILAL AANZA AWAMU YA PILI YA KAMPENI MKOA WA DODOMA

Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokelewa na wanachama na wasanii wa ngoma za asili za Kabila la Wagogo, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mkoani Dodoma leo kwa ajili ya kuanza ziara yake ya mikutano ya Kampeni baada ya mapumziko ya sikukuu ya Eid El Fitr, ambapo leo ameanza ziara hiyo katika Kanda ya Kati.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa eneo la Soko la Mahindi wakati wa mkutano wa kampeni ulioanza leo kwa mgombea huyo baada ya mapumziko ya sikukuu ya Eid.
Wasanii wa Kikundi cha ngoma ya asili cha Maomanyika, wakiwa kwenye uwanja wa Makulu wakati wakimsikiliza Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akifanya mkutano wa Kampeni mkoani Dodoma leo.
Wananchi wa Kongwa wakimsikiliza Mgombea Mwenza katika eneo la Soko la Mahindi..
Wananchi wa Mji Mdogo wa Kibaigwa Wilaya ya Kongwa, wakiwa wamesimama juu ya magunia ya Mahindi wakimsikiliza mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Umati huu ni wa Kibaigwa wao hufanya magunia ya mahindi kuwa ndiyo majukwaa yao.






No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.