Habari za Punde

*MAAJABU YA KWELI, VIBOKO MARAFIKI WA BINADAMU

Ukisikia raia wa kigeni wanaingia nchini na kulipa dola nyingi ili kujionea maajabu tuliyojaaliwa Watanzania wala usiwashangae kwa hata wewe mdau unapopata fursa ya kutembea na kufanya Utalii wa ndani unaweza kukutana na mambo kama haya ambayo hata unapokuwa ukihadithiwa unaweza usiamini na kupuuza na kubaki na akili yako kuwa hili haliwezekani. Je wewe Mdau wa Sufianimafoto, ulishawahi kusikia Kiboko ama Viboko wakawa marafiki wa Binadamu? hebu sikia hii. Katika picha hii kuna mchoro wa alama nyekundu iliyozungushiwa, katikati ya vijiduara hivi ni Viboko wakiwa katika Mto Kiasi ulipo katika Mkoa mpya wa Katavi, na kiduara kidogo (kushoto) ni binadamu wawili wa kijiji hicho wakitoka kuchota maji mtoni hapo, Viboko hao wamekuwa wakishirikiana na wananchi wa Kijiji hicho kutumia maji ya mto huo bila kuwadhuru wananchi hapo, ambapo wananchi hao huchota maji katika mto huo bila kuwaogopa Viboko hao ambao muda wote huwa eneo hilo huku wakiwa hawana habari na binadamu hao ambao nao huchota maji katika mto huo bila wasiwasi na kuondoka zao. Na muda wa usiku imeelezwa kuwa Viboko hao hutoka majini na kuingia mtaani katika mitaa ya kijiji hicho kusaka msosi na hata wanapokutana na binadamu hupishana tu kila mmoja na time yake, HAMA KWA HAKIKA URAFIKI WA NAMNA HII SI WA MASHAKA.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.