Habari za Punde

*MSAFARA WA DK.BILAL WAZUILIWA NA WANANCHI

Wananchi wa Kijiji cha Miombo Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa, wakiwa wametanda barabarani ili kumzuia mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakimtaka kusimama eneo hilo kwa lengo la kumuona na kuzungumza nao na wengine wakisikika kupiga kelele kumuomba kujua jina lake. Baada ya kusimama eneo hilo Dk. Bilal alizungumza nao na kumpa fursa mwananchi mmoja wa eneo hilo kumtaka kusema moja ya kero sugu inayowasumbua. Mwananchi huyo alipokea mic na kuzungumza bila kituo kwa kusema "Kero yetu sisi Mheshimiwa tunaomba pindi utakapofanikiwa kuwa Makamu au msaidizi wa Rais Jakaya Kikwete, tunakuomba utusaidie kutupunguzia bei za Pembejeo za Kilimo ili hata sisi wananchi wa hali ya chini tuweze kumudu kununua na kulima kwa hali zaid tuweze kukumu maisha yetu na Familia zetu" alimaza kusema na kushangiliwa na umati uliokuwapo eneo hilo.
Mgombea Mwenza Dk Mohamed Gharib Bilal na mkewe Bi Zakia Bilal, wakishangaa staili ya wasanii wa ngoma ya Kabila la Wafipa, ya mmoja kupakata Kinu na mmoja kutwanga tena kwa nguvu zote, wakati wa maokezi yake alipowasili katika Kijiji cha Mtenga Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo, Ally Kessy jana.
Baada ya hapo Msafara wa Dk. Bilal hatimaye uliingia mji wa Mpanda.
Msafara huo ulipokelewa na waendesha Pikipiki ulioongoza hadi eneo la kufanyika mkutano huo katika Kijiji cha Majalila Mpanda Ndogo katika Mkoa mpya wa Katavi.
Baadhi ya wananchama waliokuwa wa Vyma Pinzani, wakila kiapo baada ya kukabidhi Kadi zao kwa Mgombea Mwenza Dk Bilal na kukabidhiwa kadi mpya za CCM, wakati wa mkutano huo.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.