
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal, akimpa pole
Mgombea Udiwani wa Kata ya Masama Mashariki wa CCM, Dk. Ali Abeid Mwanga, akizungumza na kuonyesha jeraha alilolipata baada ya kupigwa na wapinzani Okt 14 mwaka huu wakati wapinzani hao wakipita karibu na ofisi yake kuelekea katika Kijiji jirani kufanya mkutano na kusimama eneo hilo na kumvamia katika ofisi yake na kisha kumshambulia. Diwani huyo alipanda jukwaani na kusema hayo wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipofika katika Kijiji cha Kawaya Kata ya Sama Rundugai kufanya mkutano wa kampeni.
Mashabiki na wanachama wa CCM wa Pasua Mkoani Kilimanjaro, wakimsikiliza Dk Bilal jana jioni.

Hii ni staili gani ya kusikiliza sera za mgombea? Hapa wakiwa ni miongoni mwa wasikilizaji wa sera za CCM wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza Dk. Bilal katika eneo hili la Pasua ambalo lilikuwa ni moja na ngome kabambe ya Mgombea ubunge Philemon Ndesambulo.
No comments:
Post a Comment