Habari za Punde

*DK. JAKAYA NA DK BILAL, WAFUNGA MIKUTANO YAO YA KAMPENI YA CCM

Mgombea Urais wa CCM, Dk. Jakaya Kikwete, akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu kupitia Mkoa wa Dar es Salaam, Asha Baraka, wakati akiingia kwenye viwanja vya Jangwani leo okt 30 kwa ajili ya kufunga mikutano ya kampeni.
Mgombea urais wa CCM, Dk Jakaya Kikwete, akiwahutubia wanachama wa CCM, wakati wa hafla ya kufunga mikutano ya kampeni ya CCM, iiyofanyika kwenye viwanja vya Jangwani.
Sehemu ya wanachama wa CCM na wananchi waliojitokeza kuhudhulia hafla hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni ya CCM, iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jangwani.
Mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwenye hafla ya kufunga mikutano ya kampeni iliyofanyika kwenye uwanja wa Jangwani
Kutoka (kushoto) Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, Pius Msekwa, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu na Mgombea mwenza wa CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika mkutano huo.
Kutoka (kulia) wake wa Dk Bilal, Bi Zakia Bilal na Bi Asha Bilal, wakiwa na Sophia Simba, baada ya kumalizika kwa mkutano huo. Kushoto ni Katibu wa CCM Taifa, Yusuph Makamba.

"Mie naenda Bara kupiga kura, nawe karibu upigie hapa nyumbani"
Dk Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Dk Ali Mohamed Shein, wakati walipokutano uwanja wa ndege wa Zanzibar jana jioni, wakipishana kila mmoja akielekea eneo lake la kupigia kura, ambapo Dk Shein alikuwa akielekea Oysterbay jijini Dar es Salaam, eneo alilojiandikisha kupigia kura na Dk Bilal, Visiawani Zanzibar.








No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.