
Meneja wa Hoteli ya Naura Spring, Beatrice Dalaris (katikati) akipozi na wahudumu wa hoteli hiyo katika picha, Neema Justine (kushoto) na Asteria Mathias, wakati wakijiandaa kuupokea msafara wa Mgombea mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwasili mkoani Arusha akitokea Merera, ambako alifanya mkutano wa mwisho wa kukamilisha ratiba yake ya ziara za mikutano yake leo. Meneja huyo alisema kuwa kwa kutambua mchango wa msafara huo wameamua kuandaa sare zinzoendana na msafara waliokuwa wakiupokea ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa CCM na viongozi wa msafara huo.

Baadhi ya watu walio katika msafara huo wakiingia Hotelini hapo leo jioni, kama unavyoona pichani mmoja wa wahudumu (mwanadada katikati) Neema Justine, akiwa amevalia sare inayofanana na wageni hao.
No comments:
Post a Comment