SIKU mbili tu baada ya mechi ya Kimataifa ya kusaka tiketi ya kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Mataifa baina ya timu ya Taifa (Taifa Stars) na Moroco kumalizika kuingia dosari kwa wasimamizi TFF kuaibika mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwa kushindwa kupiga wimbo wa Taifa, kwa kile kilichodaiwa Cd kugoma kupiga.
Shirikisho la Soka nchini (TFF) limemsimamisha kazi Ofisa habari wake, Florian Kaijage (pichani) kutokana na fedheha hiyo ya kushindwa kutimiza itifaki Dmuhimu ya kupiga nyimbo za Mataifa hayo mawili kabla ya kuanza kwa mtanange huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Rais wa TFF, Leodegar Tenga, amesema kuwa tukio hilo ni la aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete na mashabiki na wageni wengine waliokuwapo uwanjani hapo na kuongeza kuwa, mbaya zaidi kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi, hivyo aibu hiyo imeshuhudiwa na wapenzi wa soka dunani kote.
Aidha alisema kuwa kwa tukio hilo TFF imemua kumwajibisha Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo.
Na kuongeza kuwa baada ya Kaijage kusimamishwa atakuwa akiisaidia timu itakayoundwa kuchunguza jambo hilo na kwamba hatua zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhusika na tukio hilo.
Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mchezo na Brazil ambapo safari hii wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.
“Kushindwa upigaji nyimbo za taifa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali ni aibu kwa taifa letu, napenda kwa niaba ya tff kuomba radhi kwa Mheshiwa Rais, wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa jumla na wageni wetu kutoka Morocco” alisema tenga.
Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.
No comments:
Post a Comment