
Aliyekuwa Naibu wa Spika wa Bunge wa awamu iliyopita, ambaye pia alikuwa ni mmoja kati ya wanamama watatu waliokuwa wakiwania nafasi ya Kiti hicho, Anna Makinda (kulia) akipongezwa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azan, baada ya kutoka kwenye Ukumbi wa mikutano na kutangazwa kupitishwa jina lake kuwania nafasi hiyo, wakati alipokuwa akichuana na Anna Abdallah na Kate Kamba leo mjini Dodoma. Anna Makinda sasa atakuwa ndiye mwakilishi wa CCM katika kuwania nafasi hiyo ambapo atakuwa akichuana na Mabele Malando wa CHADEMA, baada ya wapinzani pia kumteuwa Mabele kuwania Kiti hicho.

Anna Makinda akipiga picha ya kumbukumbu na baadhi ya wabunge kwa furaha baada ya kuteuliwa jina lake kuwani Kiti cha Spika.

Anna Makinda kihojiwa na waandishi wa habari baada ya kutoka katika chumba cha mkutano.

Mwandishi Mwandamizi wa Kampuni ya New Habari Corporation, Manyerere Jackton (kulia) akipiga picha ya kumbukumbu na Anna Makinda baada ya kutangazwa mshindi kati ya majina matatu yaliyokuwa yakiwania nafasi hiyo ya kuwania Kiti cha Spika.

Anna Makinda akitoka ukumbini humo akiwa na furaha lukuki....

Anna Abdallah, akitoka ukumbini humo akiwa na huzuni baada ya jina lake kumwagwa na Anna Makinda.
No comments:
Post a Comment