Sufianimafoto Reporter, Dar
MWANAMUZIKI nyota wa barani Afrika, Bozi Boziana anatarajiwa kuwasili nchini
Novemba 25 kufanya maonyesho mawili akiwa na bendi ya African Stars maarufu,
Twanga Pepeta.
Maonyesho hayo yamepangwa kufanyika Novemba 27 kwenye ukumbi wa Mango Garden na
siku inayofuata kwenye viwanja vya Leaders Club katika bonanza la kila siku ya
Jumapili maarufu kwa jina la SSB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET),
Asha Baraka alisema jana kuwa hatua ya kufanya onyesho na mwanamuziki huyo
mkongwe inatokana na mpango wao wa kujitangaza katika soko la kimataifa.
Baraka alisema kuwa mara baada ya maonyesho hayo, wanamuziki wengine wa Bozi
Boziana wataondoka nchini na mkongwe huyo kubakia hapa nchini akiandaa albamu
mpya ambayo atairekodi akiwa na wanamuziki wa bendi yake.
Alisema kuwa albamu hiyo itakuwa na lugha mchanganyiko ya Kilingala na Kiswahili
na baada ya kukamilika utunzi wake, itakwenda kufanyiwa ‘mixing’ nchini
Ufaransa.
“Bozi Boziana ataimba Kilingala na baadhi ya maneno kuimba Kiswahili, wanamuziki
wetu watimba Kiswahili na Boziana kuimba ubeti huo huo Kilingala, lengo hapa ni
kupromoti lugha yetu kwani naamini albamu hii itauza DR- Congo na nchi
nyinginezo,” alisema Baraka.
Asha ambaye anajulikana kama mwanamke wa chuma “Iron Lady” amewaomba wadhamini
mbali mbali kujitokeza kusaidia kufanikisha kwa maonyesho hayo mawili na
maandalizi ya albamu hiyo.
Alifafanua kuwa bendi yae pia itaendelea na maandalizi ya maandalizi ya albamu
mpya ambapo mpaka sasa wamekwisha kamilika jumla ya nyimbo nne.
No comments:
Post a Comment