Habari za Punde

*YALIYOIBUKA MJINI DODOMA LEO

NAFASI YA USPIKA, SPIKA SITTA, CHENGE, CHALI, KINAMAMA WAPETA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete, akifungua Kikao cha Kamati Kuu, kilichokaa leo mjini Dodoma kujadili majina matatu yatakayowasilishwa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge.

WABUNGE WA VITI MAALUM SAFARI HII MOTO!
Wabunge wa Viti Maalum, Vicky Kamata (kushoto) akiwa na mwenzie wakiingia katika Ofisi za Bunge mjini Dodoma leo....
'WAGOMBEA WAKIWA PAMOJA WAKATI WAKISUBIRI KUCHAKACHULIWA'
Wagombea wa nafasi ya Kiti cha Spika wa Bunge, wakiwa katika picha ya pamoja katika benchi moja wakati wajumbe wa Kamati Kuu wakiwa ndani wakiendelea na zoezi la kujadili majina matatu yatakayopitishwa kuwania nafasi hiyo.
'KAMA MARAFIKI VILE KUMBE......'
Wagombea wa Kiti cha Spika, Mbunge wa Urambo Samuel Sitta na Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge, wakitoka kwa pamoja katika ukumbi uliokuwa ukifanyika majadiliano ya kupitisha majina ya wagombea wa nafasi hiyo leo mjini Dodoma.
Samuel Sitta, akitoka Ukumbini kuondoka zake baada ya jina lake kuchakachuliwa yaani kukatwa pamoja na Chenge na hatimaye yakapitishwa majina ya wagombea Kinamama ambao ni Anna Abdalla, Kate Kamba na Anne Makinda, ambao ndiyo watawania nafasi hiyo na hatimaye mmoja kati yao kuibuka na kumrithi Samuel Sitta.

"HONGERA KWA KUCHUKUA JIMBO LA KAWE"
Samuel Sitta, akisalimiana na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee wakati walipokutana kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo....
CHADEMA NAO WAKAA KUJADILI MAJINA YA VIONGOZI WAO BUNGENI
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, akiwa katika kikao cha kujadili na kupitisha majina ya wawakilishi na viongozi wao Bungeni.

SUGU NAYE ATINGA MJENGONI KAMA NDOTO
Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi A.K.A Mr ii au Sugu, akiingia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma kwa mbwembwe leo.
Sugu akimwaga mistari kwa waandishi wa habari na kuwaacha hoi, mara tu baada ya kukanyaga ardhi ya viwanja vya Bunge leo...










No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.