
Hapa ndiyo palikuwa mahala maalum pa kuchezeshea Droo hiyo katika jengo la benki hiyo lililopo Barabara ya New Bagamoyo.

Mkuu wa Bidhaa wa benki hiyo, Rwegoshora Kaijage, akifafanua jambo kuhusu Droo hiyo kabla ya kuanza kuchezeshwa.

Mfanyakazi wa Benki ya Baclays katika kitengo cha mauzo na Masoko, Jacqueline Rutatora, akiokota karatasi ya jina la mshindi wa droo ya pili ya Baclays Premier Accounts (BPL), wakati ilipokuwa ikichezesha droo hiyo leo jijini Dar es Salaam, ambapo walipatikana washindi watatu watakaokwende nchini Uingereza kushuhudia mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa. Kulia ni Msimamizi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, (katikati) ni Meneja wa Baclays Tanzania, Rahma Gemina na Mkuu wa Bidhaa, Rwegoshora Kaijage.

Caroline Mosha naye pia akiokota karatasi ndani ya kisanduku hicho kumpata mshindi wa pili.

Meneja wa Baclays Tanzania, Rahma Gemina akichezesha Droo ya pili ya Baclays Premier Accounts (BPL), wakati ilipokuwa ikichezeshwa droo hiyo leo jijini Dar es Salaam, ambapo walipatikana washindi watatu watakaokwende nchini Uingereza kushuhudia mchezo mmoja wa Ligi ya Mabingwa. Katikati ni Msimamizi kutoka Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini, Bakari Maggid, (kushoto) ni Mkuu wa Bidhaa, Rwegoshora Kaijage

Huyu pia ni mmoja kati ya wafanyakazi wa benki hiyo akizungusha kuchezesha droo hiyo kumpata mshindi wa tatu.
No comments:
Post a Comment