Habari za Punde

*DAR ALL STARS NA ZANZIBAR HEROES NGUVU SAWA

Beki wa timu ya Zanzibar Heroes, Nadir Haroub 'Canavaro' (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Dar All Stars, Kally Ongala, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana, 0-0.
Mshambuliaji wa Dar All Stars, Rashid Gumbo (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Zanzibar Heroes, Othman Ally, wakati wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Dar All Stars, Kally Ongala (kushoto) akimtoka beki wa Zanzibar Heroes, Abuu Ubwa, wakati wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa Dar All Stars, Mussa Hassan 'Mgosi' (kushoto) akimfinya beki wa Zanzibar Heroes, Othman Ally.




No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.