Habari za Punde

*MAALIM SEIF AAPISHWA KUWA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR


Na Salma Lusangi, Zanzibar

HATIMAYE Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shairif Hamad kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa serikali ya umoja wa kitaifa (GNU)
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, amemtangaza rasm Maalim Seif kuwa Makamu wa kwanza wa rsia leo na kumtaja Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa pili wa rais.
Aidha katika taarifa ya Katibu Mkuu, Abdulhamid Yahya Mzee ilisema kuwa uteuzi huo ni kwa mujibu wa kifungu cha 39 (1) (2) (3) cha Katiba ya Zanzibar.
Maalim Seif amewahi kushika nyadhifa mbali mbali, kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 akiwa katika serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na katika chama cha Mapinduzi.
Nyadhifa hizo ni Waziri Kiongozi, Waziri wa Elimu, ambapo pia aliwahi kuwa Katibu wa Idara ya Mipango na Uchumi ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kabla ya kupanda ngazi amewahi pia kufundisha shule mbali mbali za sekondari Unguja na pemba
Katika nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein amemteua Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamo wa pili wa Rais ambaye kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ndiye atakuwa mtendaji mkuu wa Serikali ya umoja wa kitaifa visiwani.
Taarifa hiyo ya Ikulu imesema uteuzi huo ulioanza jana ni kwamujibu wa Katiba ya Zanzibar kifungu cha 39 (1) (2) (6) cha Katiba ya Zanzibar.
Balozi Seif Ali Idd pia ni Mbunge wa jimbo la Kitope alikuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika serikali iliyopita ya Rais Kikwete kabla ya kuingia katika mbio za Ubunge Balozi Idd aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.
Katika hatua nyengine, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jana walifanya kikao chao cha kwanza mjini Zanzibar na kumteua, Pandu Ameir Kificho kuwa Spika wa Baraza hilo.
Spika Kificho alitangazwa mshindi baada ya kunyakuwa kura 45 dhid ya 32 alizopata mgombea wa CUF, Abas Juma Muhunzi kati ya kura 78 zilizopigwa.
Wajumbe wa CCM walikuwa 45 na wa CUF 33 na Spika alitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo ambao hakuwa na ushindani mkubwa kutokan na wana CCM kushindwa kujitokeza katika uchaguzi huo na kificho kuwa mgombea pekee wa CCM.
Spika Kificho amekamata uongozi wa Baraza hilo kuanzia mwaka 1995 na hatakuwa spika kwa kwanza kuongoza baraza lenye sura ya muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa.
Baadaye Spika Kificho aliwapa taarifa wajumbe hao kuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein atahutubia Baraza kesho.
Chimbuko la serikali ya umoja wa kitaifa imetokana maridhiano yaliyofikiwa Novemba tano mwaka jana kati ya vyama vya CCM na CUF baada ya asilimia 66 kuunga mkono mabadiliko ya katiba ya kuruhusu muundo huo wa serikali kupitia kura ya maoni.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.