
Kondakta wa daladala linalofanya safari zake Mtongani na Posta jijini Dar es Salaam, akihakiki noti ya Sh 10,000, aliyopewa na ‘Hamis Ma SMS’ (kulia) wa Kampuni ya simu za mkononi Zantel kwa ajili ya kuwalipia nauli wasafiri waliokuwa wakitoka posta kwenda Mtongani. Hamis Ma SMS leo mchana alifanya zaiara katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kutoa zawadi ikiwemo kuwalipia nauli abiria katika baadhi ya daladala kama sehemu ya kuhamasisha promosheni ya Hamis Ma SMS inayoendeshwa na kampuni hiyo.

Hamis Ma SMS (kulia) kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Zantel akimlipa kondakta nauli ya abiria wote waliokuwa ndani ya basi hilo waliokuwa wakitoka Posta kuelekea Mbagala leo mchana jijini Dar es Salaam. Hamis alifanya zaiara katika mitaa tofauti ya jiji la Dar es Salaam leo na kutoa zawadi ikiwemo ya kuwalipia nauli abiria katika daladala alilopanda ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha promosheni ya Hamis Ma SMS inayoendeshwa na kampuni hiyo.
No comments:
Post a Comment