Habari za Punde

*MAMA ASHA BILAL AZINDUA MAONYESHO YA KAZI ZA WAKE WA MABALOZI, KUCHANGIA WATU WASIOJIWEZA

Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua rasmi maonyesho ya kazi za wake wa Mabalozi, yaliyoandaliwa na Kikundi cha wake wa Mabalozi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki jijini Dar es Salaam leo
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiangalia bidhaa za Vitenge vya Nigeria katika Banda la Nigeria wakati wa Maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi, kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Wabunge wa Viti Maalum, Zainab Vullu na Halima Mamuya.

Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiangalia Vinyago katika Banda la Rwanda ‘Vinyago Shop’ . Kushoto ni Mkurugenzi wa Banda hilo, Emma Brown Kapinga, akimfafanuliwa jambo kuhusiana na Biashara hiyo, wakati wa maonyesho ya Kazi za mikono za Wake wa Mabalozi yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo.

Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akipata maelezo ya jinsi ya kuandaa Kinywaji cha Kahawa kutoka kwa Zerthun Delelegn (kushoto) na Popu McINTIRE, wakati alipotembelea Banda la Ethiopia kwenye maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo.Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Bethsaida Girls, Francisca Francis, akiwaongoza wenzake kucheza ngoma ya Kabila la Wahaya wakati wa maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi, yalioandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watu wasiojiweza, yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki.
Washiriki kutoka China wakiandaa bidhaa zao.
'USIMPIGE MWANAMKE PIGA MPIRA Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akiwa na zawadi ya mpira aliokabidhiwa na waratibu wa maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watu wasiojiweza yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi yaliyofanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki jijini Dar es Salaam leo Nov 20. Mpira huo ulikuwa na Ujumbe usemao ‘USIMPIGE MWANAMKE PIGA MPIRA’
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal, akivishwa beji ya kampeni ya kutokomeza ugonjwa wa Vistula na mwakilishi wa ‘MABINTI Vistula’, Katia Geurts, kutoka CCBRT, wakati alipoalikwa kufungua rasmi maonyesho ya Kazi za Wake wa Mabalozi yaliyoandaliwa na Kikundi cha Wake wa Mabalozi nchini kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasaidia watoto na watu wasiojiweza na NGO’s, yaliyofanyika kwenye Viwaanja vya Shule ya Tanganyika International Masaki Jijini Dar es Salaam leo.
Meriam Nganahe, akiwa katika Banda lake la Maonyesho hayo la Namibia, akipanga bidhaa zake kabla ya kufunguliwa rasmi.
Miongoni mwa washiriki wa maonyesho hayo kutoka nchini Russia, wakiandaa bidhaa zao.









No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.