Habari za Punde

*MAMIA WAMUAGA SILLERSAID MZIRAY DAR

Jeneza lenye mwili wa marehemu Sillersaid Mziray, liki katika Viwanja vya Biafra wakati wa shughuli za mazishi leo.
Mwanamuziki wa zamani, Kassim Mapili, akinama kubusu mwili wa aliyekuwa Kocha wa Viungo wa Klabu ya Simba, Sillersaid Mziray, ikiwa ni ishara ya kuaga wakati wa shughuli za mazishi zilizofanyika kwenye Viwanja vya Biafra Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Leodger Tenga akiwa ni miongoni mwa watu waliofika kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Kocha wa viungo wa Klabu ya Simba Sillersaid Mziray wakati wa shughuli za mazishi zilizofanyika kwenye Viwanja vya Biafra leo mchana.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, akisoma risala kwa niaba ya Klabu hiyo wakati wa shughuli hiyo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari za michezo Tanzania, Juma Pinto, akisoma risala kwa niaba ya waandishi wa habari wakati wa shughuli hiyo.





No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.