Askari wa kutuliza ghasia (FFU) wakiwatuliza mashabiki wa CHADEMA, waliokuwa wamekusanyika katika Kituo cha kupigia kura cha Loyola Mabibo leo mchana, wakisubiri kutangazwa matokeo ya kura ya kituo hicho, ambapo waliahidi kutoondoka kituoni hapo hadi yatakapotangazwa matokeo hayo. Mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuhamasisha kutolewa kwa matokeo hayo.
Mashabiki hao wakiwa na mabango mahala hapo wakati wakisubiri kutolewa kwa matokeo hayo, ambapo walikuwa wakiamini kuwa mgombea wao Mnyika ndiye ataibuka kidedea.

Mashabiki hao wakisebeneka kwa nyimbo na ngoma mahala hapo wakati wakisubiri matokeo hayo.

Baadhi yao wakisikiliza matangazo ya matokeo katika vituo vingine katika redio iliyokuwa ikitangaza katika moja ya gari lililokuwa jirani hapo.
No comments:
Post a Comment