Habari za Punde

*PAPA MUSOFE ADHAMINI SHINDANO LA MISS UTALII KWA M.120

Shindano la Miss Utalii Tanzania 2010 linalotarajia kufanyika Desemba 31 mwaka huu sasa kufanyika kwa udhamini wa Sh. Milioni 120, fedha zilizotolewa na 'Papa Musofe'.

Akizungumza na gazeti hili Rais na Mratibu wa mashindano hayo, Gideon Chipungahelo, alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Kilomo iliyopo Bagamoyo, tayari yamekwishakamilika.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha shindano hilo, Kampuni ya Aucland Tours & Safaris, inayomilikiwa na Marijani Msofe ‘Papa Musofe’, tayari imekwisha tangaza kudhamini shindano hilo kwa Sh. Milioni 120.

Aidha alisema kuwa washiriki watakaopanda jukwaani siku hiyo kuwania Taiji la Miss Utalii 2011 ni 60, ambao wametoka mikoa yote ya Tanzania, ambao bado wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na shindano hilo katika Hoteli ya Kilomo.

Alifafanua udhamini huo wa Sh. Milioni 120 kuwa utakuwa ni fedha taslimu, zawadi za washiriki na kuwaandaa warembo watakaokwenda kushiriki katika mashindano ya Dunia 2011 yanatotarajia kufanyika Novemba 2011 nchini Jamaica.

Mashindano mengine ni Miss University Africa 2011 yatakayofanyika mwezi February, nchini Nigeria, Mashindano ya Miss Globe International 2011 yatakayofanyika Uturuki mwezi April, pamoja na mashindano ya International Miss Tourism, yatakayofanyika mwezi Mei Marekani.

Aliwataja wadhamni wengine kuwa ni pamoja na Tanapa, Kilomo Hotel, Ngorongoro, Image Masters & Click Photo Promotions.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.