
Kipa wa timu Simba, Juma Kaseja (wa pili kushoto) akisalimiana na mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu wa watani wa jadi, Simba na Yanga, uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza. Hivi karibuni kipa huyo apewa adhabu na Shirikisho la Soka TFF ambayo bado anaitumikia hadi hivi leo ya kutocheza michezo mitatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutokana na kile kinachodaiwa kutosalimiana na mgeni rasmi wakati wa mchezo huo, ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kupitia picha kama hii anavyoonekana akipeana mkono na mgeni rasmi, Sasa sijui uwanjani hapo alikuwapo mgeni rasmi mwingine zaidi ya huyu? mie sijui kwa hili Kamisaa na Shirikisho mmenaniliu.....
No comments:
Post a Comment