Habari za Punde

*DEREVA WA FUSO LILILOGONGANA NA GARI LA MAREHEMU SALOME MBATIA ATIWA NGUVUNI

Daud Mangulla ambaye alikuwa dereva wa gari aina ya Fuso iliyogongana na gari la Naibu Waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia (marehemu) akiwa chini ya ulinzi wa polisi, wakati akihojiwa baada ya kukamatwa mkoani Iringa jana.
Hivi ndivyo lilivyokuwa gari la marehemu Salome baada ya kugongwa.

Baada ya kupita miaka mitatu na miezi miwili tangu ilipotokea ajali iliyosababisha kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri wa Wanawake, Jinsia na Watoto marehemu Salome Mbatia hatimaye dereva wa gari hilo aina ya Fuso amekamatwa na anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka.
Ajaili hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajiri T 724 AGZ Nissan Patrol alilokuwa akitumia marehemu na Fuso ilisababisha vifo vya watu watatu na majeruhi wawili, Dereva aliyekuwa akiendesha Fuso aliingia mitini na kutokomea kusokojulikana hadi alipotiwa nguvuni jana.
Jeshi la polisi mkoani Iringa lilifanikiwa kumkamata dereva huyo ambaye amedaiwa alikimbilia porini na kuendelea na shughuli zake kwa siku zote na kurejea mjini kinyemela hadi alipokamatwa jana eneo la Stendi ya Mabasi ya Makambako baada ya taarifa ya raiawema kuwafikia Polisi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema kuwa dereva huyo wa Fuso lenye namba T 299 AFJ ,Daud Mangulla (28) mkazi wa mjimwema makambako wilaya ya Njombe anatarajia kufikishwa Mahakamani hivi karibuni baada ya kukamilika kwa taratibu zote.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.